Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

90 Al-Balad ٱلْبَلَد

< Previous   20 Āyah   The City      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

90:1 لَآ أُقْسِمُ بِهَـٰذَا ٱلْبَلَدِ
90:1 Naapa kwa Mji huu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:2 وَأَنتَ حِلٌّۢ بِهَـٰذَا ٱلْبَلَدِ
90:2 Nawe unaukaa Mji huu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:3 وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ
90:3 Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:4 لَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ فِى كَبَدٍ
90:4 Hakika tumemuumba mtu katika taabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:5 أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ
90:5 Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:6 يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا
90:6 Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:7 أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ
90:7 Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:8 أَلَمْ نَجْعَل لَّهُۥ عَيْنَيْنِ
90:8 Kwani hatukumpa macho mawili? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:9 وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ
90:9 Na ulimi, na midomo miwili? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:10 وَهَدَيْنَـٰهُ ٱلنَّجْدَيْنِ
90:10 Na tukambainishia zote njia mbili? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:11 فَلَا ٱقْتَحَمَ ٱلْعَقَبَةَ
90:11 Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:12 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْعَقَبَةُ
90:12 Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:13 فَكُّ رَقَبَةٍ
90:13 Kumkomboa mtumwa; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:14 أَوْ إِطْعَـٰمٌ فِى يَوْمٍ ذِى مَسْغَبَةٍ
90:14 Au kumlisha siku ya njaa - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:15 يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ
90:15 Yatima aliye jamaa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:16 أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ
90:16 Au masikini aliye vumbini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:17 ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَتَوَاصَوْا۟ بِٱلصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا۟ بِٱلْمَرْحَمَةِ
90:17 Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:18 أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَيْمَنَةِ
90:18 Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:19 وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا هُمْ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَشْـَٔمَةِ
90:19 Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

90:20 عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌۢ
90:20 Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)