Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

75 Al-Qiyāmah ٱلْقِيَامَة

< Previous   40 Āyah   The Resurrection      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

75:1 لَآ أُقْسِمُ بِيَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ
75:1 Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:2 وَلَآ أُقْسِمُ بِٱلنَّفْسِ ٱللَّوَّامَةِ
75:2 Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:3 أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَـٰنُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُۥ
75:3 Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:4 بَلَىٰ قَـٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّىَ بَنَانَهُۥ
75:4 Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:5 بَلْ يُرِيدُ ٱلْإِنسَـٰنُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُۥ
75:5 Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:6 يَسْـَٔلُ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلْقِيَـٰمَةِ
75:6 Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:7 فَإِذَا بَرِقَ ٱلْبَصَرُ
75:7 Basi jicho litapo dawaa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:8 وَخَسَفَ ٱلْقَمَرُ
75:8 Na mwezi utapo patwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:9 وَجُمِعَ ٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ
75:9 Na likakusanywa jua na mwezi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:10 يَقُولُ ٱلْإِنسَـٰنُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ ٱلْمَفَرُّ
75:10 Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:11 كَلَّا لَا وَزَرَ
75:11 La! Hapana pa kukimbilia! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:12 إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمُسْتَقَرُّ
75:12 Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:13 يُنَبَّؤُا۟ ٱلْإِنسَـٰنُ يَوْمَئِذٍۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ
75:13 Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:14 بَلِ ٱلْإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ بَصِيرَةٌ
75:14 Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:15 وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ
75:15 Na ingawa atatoa chungu ya udhuru. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:16 لَا تُحَرِّكْ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِۦٓ
75:16 Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:17 إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُۥ وَقُرْءَانَهُۥ
75:17 Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:18 فَإِذَا قَرَأْنَـٰهُ فَٱتَّبِعْ قُرْءَانَهُۥ
75:18 Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:19 ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُۥ
75:19 Kisha ni juu yetu kuubainisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:20 كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ ٱلْعَاجِلَةَ
75:20 Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:21 وَتَذَرُونَ ٱلْـَٔاخِرَةَ
75:21 Na mnaacha maisha ya Akhera. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:22 وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ
75:22 Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:23 إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ
75:23 Zinamwangallia Mola wao Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:24 وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍۭ بَاسِرَةٌ
75:24 Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:25 تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ
75:25 Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:26 كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِىَ
75:26 La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:27 وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ
75:27 Na pakasemwa: Nani wa kumganga? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:28 وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلْفِرَاقُ
75:28 Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:29 وَٱلْتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ
75:29 Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:30 إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمَسَاقُ
75:30 Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:31 فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ
75:31 Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:32 وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
75:32 Bali alikanusha, na akageuka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:33 ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ
75:33 Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:34 أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ
75:34 Ole wako, ole wako! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:35 ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰٓ
75:35 Kisha Ole wako, ole wako! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:36 أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَـٰنُ أَن يُتْرَكَ سُدًى
75:36 Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:37 أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِىٍّ يُمْنَىٰ
75:37 Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:38 ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ
75:38 Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:39 فَجَعَلَ مِنْهُ ٱلزَّوْجَيْنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰٓ
75:39 Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

75:40 أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَـٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحْـِۧىَ ٱلْمَوْتَىٰ
75:40 Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)