Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

44 Ad-Dukhān ٱلدُّخَان

< Previous   59 Āyah   The Smoke      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

44:1 حمٓ
44:1 H'a Mim - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:2 وَٱلْكِتَـٰبِ ٱلْمُبِينِ
44:2 Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:3 إِنَّآ أَنزَلْنَـٰهُ فِى لَيْلَةٍ مُّبَـٰرَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ
44:3 Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:4 فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ
44:4 Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:5 أَمْرًا مِّنْ عِندِنَآ ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ
44:5 Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:6 رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ
44:6 Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:7 رَبِّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَآ ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
44:7 Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:8 لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْىِۦ وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ
44:8 Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:9 بَلْ هُمْ فِى شَكٍّ يَلْعَبُونَ
44:9 Lakini wao wanacheza katika shaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:10 فَٱرْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِى ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ
44:10 Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:11 يَغْشَى ٱلنَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ
44:11 Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:12 رَّبَّنَا ٱكْشِفْ عَنَّا ٱلْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ
44:12 Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:13 أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَآءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ
44:13 Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:14 ثُمَّ تَوَلَّوْا۟ عَنْهُ وَقَالُوا۟ مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ
44:14 Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:15 إِنَّا كَاشِفُوا۟ ٱلْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَآئِدُونَ
44:15 Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:16 يَوْمَ نَبْطِشُ ٱلْبَطْشَةَ ٱلْكُبْرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ
44:16 Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:17 ۞ وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَآءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ
44:17 Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:18 أَنْ أَدُّوٓا۟ إِلَىَّ عِبَادَ ٱللَّهِ ۖ إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ
44:18 Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:19 وَأَن لَّا تَعْلُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ ۖ إِنِّىٓ ءَاتِيكُم بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ
44:19 Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:20 وَإِنِّى عُذْتُ بِرَبِّى وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ
44:20 Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:21 وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا۟ لِى فَٱعْتَزِلُونِ
44:21 Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:22 فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ
44:22 Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:23 فَأَسْرِ بِعِبَادِى لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ
44:23 Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:24 وَٱتْرُكِ ٱلْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ
44:24 Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:25 كَمْ تَرَكُوا۟ مِن جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
44:25 Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:26 وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ
44:26 Na mimea na vyeo vitukufu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:27 وَنَعْمَةٍ كَانُوا۟ فِيهَا فَـٰكِهِينَ
44:27 Na neema walizo kuwa wakijistareheshea! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:28 كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَـٰهَا قَوْمًا ءَاخَرِينَ
44:28 Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:29 فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلْأَرْضُ وَمَا كَانُوا۟ مُنظَرِينَ
44:29 La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:30 وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ مِنَ ٱلْعَذَابِ ٱلْمُهِينِ
44:30 Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:31 مِن فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَالِيًا مِّنَ ٱلْمُسْرِفِينَ
44:31 Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:32 وَلَقَدِ ٱخْتَرْنَـٰهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى ٱلْعَـٰلَمِينَ
44:32 Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:33 وَءَاتَيْنَـٰهُم مِّنَ ٱلْـَٔايَـٰتِ مَا فِيهِ بَلَـٰٓؤٌا۟ مُّبِينٌ
44:33 Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:34 إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَيَقُولُونَ
44:34 Hakika hawa wanasema: - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:35 إِنْ هِىَ إِلَّا مَوْتَتُنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ
44:35 Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:36 فَأْتُوا۟ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
44:36 Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:37 أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَـٰهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ مُجْرِمِينَ
44:37 Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:38 وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَـٰعِبِينَ
44:38 Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:39 مَا خَلَقْنَـٰهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
44:39 Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:40 إِنَّ يَوْمَ ٱلْفَصْلِ مِيقَـٰتُهُمْ أَجْمَعِينَ
44:40 Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:41 يَوْمَ لَا يُغْنِى مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْـًٔا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ
44:41 Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:42 إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
44:42 Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:43 إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ
44:43 Hakika Mti wa Zaqqum, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:44 طَعَامُ ٱلْأَثِيمِ
44:44 Ni chakula cha mwenye dhambi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:45 كَٱلْمُهْلِ يَغْلِى فِى ٱلْبُطُونِ
44:45 Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:46 كَغَلْىِ ٱلْحَمِيمِ
44:46 Kama kutokota kwa maji ya moto. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:47 خُذُوهُ فَٱعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ
44:47 (Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:48 ثُمَّ صُبُّوا۟ فَوْقَ رَأْسِهِۦ مِنْ عَذَابِ ٱلْحَمِيمِ
44:48 Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:49 ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْكَرِيمُ
44:49 Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:50 إِنَّ هَـٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمْتَرُونَ
44:50 Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:51 إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى مَقَامٍ أَمِينٍ
44:51 Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:52 فِى جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
44:52 Katika mabustani na chemchem, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:53 يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَـٰبِلِينَ
44:53 Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:54 كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَـٰهُم بِحُورٍ عِينٍ
44:54 Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:55 يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَـٰكِهَةٍ ءَامِنِينَ
44:55 Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:56 لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلْمَوْتَ إِلَّا ٱلْمَوْتَةَ ٱلْأُولَىٰ ۖ وَوَقَىٰهُمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ
44:56 Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:57 فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ
44:57 Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:58 فَإِنَّمَا يَسَّرْنَـٰهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
44:58 Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

44:59 فَٱرْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ
44:59 Ngoja tu, na wao wangoje pia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)