Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

79 An-Nāzi`āt ٱلنَّازِعَات

< Previous   46 Āyah   Those who drag forth      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

79:1 وَٱلنَّـٰزِعَـٰتِ غَرْقًا
79:1 Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:2 وَٱلنَّـٰشِطَـٰتِ نَشْطًا
79:2 Na kwa wanao toa kwa upole, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:3 وَٱلسَّـٰبِحَـٰتِ سَبْحًا
79:3 Na wanao ogelea, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:4 فَٱلسَّـٰبِقَـٰتِ سَبْقًا
79:4 Wakishindana mbio, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:5 فَٱلْمُدَبِّرَٰتِ أَمْرًا
79:5 Wakidabiri mambo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:6 يَوْمَ تَرْجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ
79:6 Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:7 تَتْبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ
79:7 Kifuate cha kufuatia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:8 قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ
79:8 Siku hiyo nyoyo zitapiga piga, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:9 أَبْصَـٰرُهَا خَـٰشِعَةٌ
79:9 Macho yatainama chini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:10 يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِى ٱلْحَافِرَةِ
79:10 Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:11 أَءِذَا كُنَّا عِظَـٰمًا نَّخِرَةً
79:11 Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:12 قَالُوا۟ تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ
79:12 Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:13 فَإِنَّمَا هِىَ زَجْرَةٌ وَٰحِدَةٌ
79:13 Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:14 فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ
79:14 Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:15 هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
79:15 Je! Imekufikia hadithi ya Musa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:16 إِذْ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلْوَادِ ٱلْمُقَدَّسِ طُوًى
79:16 Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia: - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:17 ٱذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
79:17 Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:18 فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ
79:18 Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:19 وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ
79:19 Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:20 فَأَرَىٰهُ ٱلْـَٔايَةَ ٱلْكُبْرَىٰ
79:20 Basi alimwonyesha Ishara kubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:21 فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
79:21 Lakini aliikadhibisha na akaasi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:22 ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ
79:22 Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:23 فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
79:23 Akakusanya watu akanadi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:24 فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلْأَعْلَىٰ
79:24 Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:25 فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلْـَٔاخِرَةِ وَٱلْأُولَىٰٓ
79:25 Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:26 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰٓ
79:26 Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:27 ءَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُ ۚ بَنَىٰهَا
79:27 Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:28 رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّىٰهَا
79:28 Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:29 وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَىٰهَا
79:29 Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:30 وَٱلْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ
79:30 Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:31 أَخْرَجَ مِنْهَا مَآءَهَا وَمَرْعَىٰهَا
79:31 Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:32 وَٱلْجِبَالَ أَرْسَىٰهَا
79:32 Na milima akaisimamisha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:33 مَتَـٰعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَـٰمِكُمْ
79:33 Kwa nafuu yenu na mifugo yenu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:34 فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلْكُبْرَىٰ
79:34 Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:35 يَوْمَ يَتَذَكَّرُ ٱلْإِنسَـٰنُ مَا سَعَىٰ
79:35 Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:36 وَبُرِّزَتِ ٱلْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ
79:36 Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:37 فَأَمَّا مَن طَغَىٰ
79:37 Basi ama yule aliye zidi ujeuri, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:38 وَءَاثَرَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا
79:38 Na akakhiari maisha ya dunia, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:39 فَإِنَّ ٱلْجَحِيمَ هِىَ ٱلْمَأْوَىٰ
79:39 Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:40 وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفْسَ عَنِ ٱلْهَوَىٰ
79:40 Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:41 فَإِنَّ ٱلْجَنَّةَ هِىَ ٱلْمَأْوَىٰ
79:41 Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:42 يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَىٰهَا
79:42 Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:43 فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَىٰهَآ
79:43 Una nini wewe hata uitaje? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:44 إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ
79:44 Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:45 إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَىٰهَا
79:45 Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

79:46 كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوٓا۟ إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَىٰهَا
79:46 Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)