Selected
Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani
Abdullah Yusuf Ali
Abdul Majid Daryabadi
Abul Ala Maududi
Ahmed Ali
Ahmed Raza Khan
A. J. Arberry
Ali Quli Qarai
Hasan al-Fatih Qaribullah and Ahmad Darwish
Mohammad Habib Shakir
Mohammed Marmaduke William Pickthall
Muhammad Sarwar
Muhammad Taqi-ud-Din al-Hilali and Muhammad Muhsin Khan
Safi-ur-Rahman al-Mubarakpuri
Saheeh International
Talal Itani
Transliteration
Wahiduddin Khan
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.
37:1
وَٱلصَّـٰٓفَّـٰتِ صَفًّا
37:1
Naapa kwa wanao jipanga kwa safu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:2
فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجْرًا
37:2
Na kwa wenye kukataza mabaya. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:3
فَٱلتَّـٰلِيَـٰتِ ذِكْرًا
37:3
Na kwa wenye kusoma Ukumbusho. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:4
إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَٰحِدٌ
37:4
Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:5
رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ ٱلْمَشَـٰرِقِ
37:5
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:6
إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِزِينَةٍ ٱلْكَوَاكِبِ
37:6
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:7
وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَـٰنٍ مَّارِدٍ
37:7
Na kulinda na kila shet'ani a'si. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:8
لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ
37:8
Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:9
دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ
37:9
Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:10
إِلَّا مَنْ خَطِفَ ٱلْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُۥ شِهَابٌ ثَاقِبٌ
37:10
Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:11
فَٱسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَآ ۚ إِنَّا خَلَقْنَـٰهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍۭ
37:11
Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:12
بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ
37:12
Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:13
وَإِذَا ذُكِّرُوا۟ لَا يَذْكُرُونَ
37:13
Na wanapo kumbushwa hawakumbuki. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:14
وَإِذَا رَأَوْا۟ ءَايَةً يَسْتَسْخِرُونَ
37:14
Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:15
وَقَالُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ
37:15
Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:16
أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ
37:16
Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:17
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلْأَوَّلُونَ
37:17
Hata baba zetu wa zamani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:18
قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَٰخِرُونَ
37:18
Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:19
فَإِنَّمَا هِىَ زَجْرَةٌ وَٰحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ
37:19
Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:20
وَقَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ ٱلدِّينِ
37:20
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:21
هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
37:21
Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:22
۞ ٱحْشُرُوا۟ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ وَأَزْوَٰجَهُمْ وَمَا كَانُوا۟ يَعْبُدُونَ
37:22
Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu - - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:23
مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْجَحِيمِ
37:23
Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:24
وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْـُٔولُونَ
37:24
Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa: - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:25
مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ
37:25
Mna nini? Mbona hamsaidiani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:26
بَلْ هُمُ ٱلْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ
37:26
Bali hii leo, watasalimu amri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:27
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ
37:27
Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:28
قَالُوٓا۟ إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ ٱلْيَمِينِ
37:28
Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:29
قَالُوا۟ بَل لَّمْ تَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ
37:29
Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:30
وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَـٰنٍۭ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَـٰغِينَ
37:30
Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:31
فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَآ ۖ إِنَّا لَذَآئِقُونَ
37:31
Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:32
فَأَغْوَيْنَـٰكُمْ إِنَّا كُنَّا غَـٰوِينَ
37:32
Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:33
فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِى ٱلْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ
37:33
Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:34
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ
37:34
Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:35
إِنَّهُمْ كَانُوٓا۟ إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ
37:35
Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:36
وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓا۟ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍۭ
37:36
Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:37
بَلْ جَآءَ بِٱلْحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلْمُرْسَلِينَ
37:37
Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:38
إِنَّكُمْ لَذَآئِقُوا۟ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَلِيمِ
37:38
Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:39
وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
37:39
Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:40
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
37:40
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:41
أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ
37:41
Hao ndio watakao pata riziki maalumu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:42
فَوَٰكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ
37:42
Matunda, nao watahishimiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:43
فِى جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ
37:43
Katika Bustani za neema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:44
عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَـٰبِلِينَ
37:44
Wako juu ya viti wamekabiliana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:45
يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍۭ
37:45
Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:46
بَيْضَآءَ لَذَّةٍ لِّلشَّـٰرِبِينَ
37:46
Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:47
لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ
37:47
Hakina madhara, wala hakiwaleweshi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:48
وَعِندَهُمْ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ عِينٌ
37:48
Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:49
كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ
37:49
Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:50
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ
37:50
Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:51
قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّى كَانَ لِى قَرِينٌ
37:51
Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:52
يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُصَدِّقِينَ
37:52
Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:53
أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ
37:53
Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:54
قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ
37:54
Atasema: Je! Nyie mnawaona? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:55
فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِى سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ
37:55
Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:56
قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ
37:56
Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:57
وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّى لَكُنتُ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ
37:57
Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:58
أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ
37:58
Je! Sisi hatutakufa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:59
إِلَّا مَوْتَتَنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ
37:59
Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:60
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ
37:60
Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:61
لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ ٱلْعَـٰمِلُونَ
37:61
Kwa mfano wa haya nawatende watendao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:62
أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ
37:62
Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:63
إِنَّا جَعَلْنَـٰهَا فِتْنَةً لِّلظَّـٰلِمِينَ
37:63
Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:64
إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِىٓ أَصْلِ ٱلْجَحِيمِ
37:64
Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:65
طَلْعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَـٰطِينِ
37:65
Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:66
فَإِنَّهُمْ لَـَٔاكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِـُٔونَ مِنْهَا ٱلْبُطُونَ
37:66
Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:67
ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ
37:67
Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:68
ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى ٱلْجَحِيمِ
37:68
Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:69
إِنَّهُمْ أَلْفَوْا۟ ءَابَآءَهُمْ ضَآلِّينَ
37:69
Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:70
فَهُمْ عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِمْ يُهْرَعُونَ
37:70
Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:71
وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ ٱلْأَوَّلِينَ
37:71
Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:72
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ
37:72
Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:73
فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُنذَرِينَ
37:73
Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:74
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
37:74
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:75
وَلَقَدْ نَادَىٰنَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ ٱلْمُجِيبُونَ
37:75
Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:76
وَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ
37:76
Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:77
وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلْبَاقِينَ
37:77
Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:78
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
37:78
Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:79
سَلَـٰمٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِى ٱلْعَـٰلَمِينَ
37:79
Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:80
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
37:80
Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:81
إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ
37:81
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:82
ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ
37:82
Kisha tukawazamisha wale wengine. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:83
۞ وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبْرَٰهِيمَ
37:83
Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:84
إِذْ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ
37:84
Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:85
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَاذَا تَعْبُدُونَ
37:85
Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:86
أَئِفْكًا ءَالِهَةً دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ
37:86
Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:87
فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
37:87
Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:88
فَنَظَرَ نَظْرَةً فِى ٱلنُّجُومِ
37:88
Kisha akapiga jicho kutazama nyota. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:89
فَقَالَ إِنِّى سَقِيمٌ
37:89
Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:90
فَتَوَلَّوْا۟ عَنْهُ مُدْبِرِينَ
37:90
Nao wakamwacha, wakampa kisogo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:91
فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ
37:91
Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:92
مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ
37:92
Mna nini hata hamsemi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:93
فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًۢا بِٱلْيَمِينِ
37:93
Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:94
فَأَقْبَلُوٓا۟ إِلَيْهِ يَزِفُّونَ
37:94
Basi wakamjia upesi upesi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:95
قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ
37:95
Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:96
وَٱللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ
37:96
Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:97
قَالُوا۟ ٱبْنُوا۟ لَهُۥ بُنْيَـٰنًا فَأَلْقُوهُ فِى ٱلْجَحِيمِ
37:97
Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:98
فَأَرَادُوا۟ بِهِۦ كَيْدًا فَجَعَلْنَـٰهُمُ ٱلْأَسْفَلِينَ
37:98
Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:99
وَقَالَ إِنِّى ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّى سَيَهْدِينِ
37:99
Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:100
رَبِّ هَبْ لِى مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
37:100
Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:101
فَبَشَّرْنَـٰهُ بِغُلَـٰمٍ حَلِيمٍ
37:101
Basi tukambashiria mwana aliye mpole. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:102
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعْىَ قَالَ يَـٰبُنَىَّ إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلْمَنَامِ أَنِّىٓ أَذْبَحُكَ فَٱنظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَـٰٓأَبَتِ ٱفْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
37:102
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:103
فَلَمَّآ أَسْلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلْجَبِينِ
37:103
Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:104
وَنَـٰدَيْنَـٰهُ أَن يَـٰٓإِبْرَٰهِيمُ
37:104
Tulimwita: Ewe Ibrahim! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:105
قَدْ صَدَّقْتَ ٱلرُّءْيَآ ۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
37:105
Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:106
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْبَلَـٰٓؤُا۟ ٱلْمُبِينُ
37:106
Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:107
وَفَدَيْنَـٰهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ
37:107
Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:108
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
37:108
Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:109
سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ
37:109
Iwe salama kwa Ibrahim! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:110
كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
37:110
Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:111
إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ
37:111
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:112
وَبَشَّرْنَـٰهُ بِإِسْحَـٰقَ نَبِيًّا مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
37:112
Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:113
وَبَـٰرَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰٓ إِسْحَـٰقَ ۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ مُبِينٌ
37:113
Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:114
وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ
37:114
Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:115
وَنَجَّيْنَـٰهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ
37:115
Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:116
وَنَصَرْنَـٰهُمْ فَكَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَـٰلِبِينَ
37:116
Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:117
وَءَاتَيْنَـٰهُمَا ٱلْكِتَـٰبَ ٱلْمُسْتَبِينَ
37:117
Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:118
وَهَدَيْنَـٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ
37:118
Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:119
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
37:119
Na tukawaachia (sifa njema) katika watu walio kuja baadaye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:120
سَلَـٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ
37:120
Iwe salama kwa Musa na Haruni! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:121
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
37:121
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:122
إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ
37:122
Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:123
وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
37:123
Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:124
إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ
37:124
Alipo waambia watu wake: Hamwogopi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:125
أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ ٱلْخَـٰلِقِينَ
37:125
Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:126
ٱللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ
37:126
Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:127
فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ
37:127
Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:128
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
37:128
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:129
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
37:129
Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:130
سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِلْ يَاسِينَ
37:130
Iwe salama kwa Ilyas. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:131
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
37:131
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:132
إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ
37:132
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:133
وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
37:133
Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:134
إِذْ نَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ أَجْمَعِينَ
37:134
Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:135
إِلَّا عَجُوزًا فِى ٱلْغَـٰبِرِينَ
37:135
Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:136
ثُمَّ دَمَّرْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ
37:136
Kisha tukawaangamiza wale wengineo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:137
وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ
37:137
Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:138
وَبِٱلَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
37:138
Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:139
وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
37:139
Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:140
إِذْ أَبَقَ إِلَى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ
37:140
Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:141
فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُدْحَضِينَ
37:141
Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:142
فَٱلْتَقَمَهُ ٱلْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ
37:142
Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:143
فَلَوْلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُسَبِّحِينَ
37:143
Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:144
لَلَبِثَ فِى بَطْنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
37:144
Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:145
۞ فَنَبَذْنَـٰهُ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٌ
37:145
Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:146
وَأَنۢبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ
37:146
Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:147
وَأَرْسَلْنَـٰهُ إِلَىٰ مِا۟ئَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ
37:147
Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:148
فَـَٔامَنُوا۟ فَمَتَّعْنَـٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍ
37:148
Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:149
فَٱسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ ٱلْبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلْبَنُونَ
37:149
Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:150
أَمْ خَلَقْنَا ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ إِنَـٰثًا وَهُمْ شَـٰهِدُونَ
37:150
Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:151
أَلَآ إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ
37:151
Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema: - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:152
وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ
37:152
Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:153
أَصْطَفَى ٱلْبَنَاتِ عَلَى ٱلْبَنِينَ
37:153
Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:154
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ
37:154
Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:155
أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
37:155
Hamkumbuki? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:156
أَمْ لَكُمْ سُلْطَـٰنٌ مُّبِينٌ
37:156
Au mnayo hoja iliyo wazi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:157
فَأْتُوا۟ بِكِتَـٰبِكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
37:157
Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:158
وَجَعَلُوا۟ بَيْنَهُۥ وَبَيْنَ ٱلْجِنَّةِ نَسَبًا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ ٱلْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ
37:158
Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:159
سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ
37:159
Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:160
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
37:160
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:161
فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ
37:161
Basi hakika nyinyi na mnao waabudu - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:162
مَآ أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَـٰتِنِينَ
37:162
Hamwezi kuwapoteza - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:163
إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ ٱلْجَحِيمِ
37:163
Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:164
وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ
37:164
Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:165
وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلصَّآفُّونَ
37:165
Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:166
وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلْمُسَبِّحُونَ
37:166
Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:167
وَإِن كَانُوا۟ لَيَقُولُونَ
37:167
Na walikuwapo walio kuwa wakisema: - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:168
لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ
37:168
Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:169
لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
37:169
Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:170
فَكَفَرُوا۟ بِهِۦ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
37:170
Lakini waliukataa. Basi watakuja jua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:171
وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلْمُرْسَلِينَ
37:171
Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:172
إِنَّهُمْ لَهُمُ ٱلْمَنصُورُونَ
37:172
Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:173
وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ
37:173
Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:174
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ
37:174
Basi waachilie mbali kwa muda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:175
وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ
37:175
Na watazame, nao wataona. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:176
أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ
37:176
Je! Wanaihimiza adhabu yetu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:177
فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلْمُنذَرِينَ
37:177
Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:178
وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ
37:178
Na waache kwa muda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:179
وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ
37:179
Na tazama, na wao wataona. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:180
سُبْحَـٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ
37:180
Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:181
وَسَلَـٰمٌ عَلَى ٱلْمُرْسَلِينَ
37:181
Na Salamu juu ya Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
37:182
وَٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
37:182
Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)