Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

93 Ađ-Đuĥaá ٱلضُّحَىٰ

< Previous   11 Āyah   The Morning Hours      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

93:1 وَٱلضُّحَىٰ
93:1 Naapa kwa mchana! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:2 وَٱلَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ
93:2 Na kwa usiku unapo tanda! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:3 مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ
93:3 Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:4 وَلَلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ ٱلْأُولَىٰ
93:4 Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:5 وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰٓ
93:5 Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:6 أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَـَٔاوَىٰ
93:6 Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:7 وَوَجَدَكَ ضَآلًّا فَهَدَىٰ
93:7 Na akakukuta umepotea akakuongoa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:8 وَوَجَدَكَ عَآئِلًا فَأَغْنَىٰ
93:8 Akakukuta mhitaji akakutosheleza? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:9 فَأَمَّا ٱلْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ
93:9 Basi yatima usimwonee! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:10 وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنْهَرْ
93:10 Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

93:11 وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ
93:11 Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)