Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

81 At-Takwīr ٱلتَّكْوِير

< Previous   29 Āyah   The Overthrowing      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

81:1 إِذَا ٱلشَّمْسُ كُوِّرَتْ
81:1 Jua litakapo kunjwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:2 وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتْ
81:2 Na nyota zikazimwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:3 وَإِذَا ٱلْجِبَالُ سُيِّرَتْ
81:3 Na milima ikaondolewa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:4 وَإِذَا ٱلْعِشَارُ عُطِّلَتْ
81:4 Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:5 وَإِذَا ٱلْوُحُوشُ حُشِرَتْ
81:5 Na wanyama wa mwituni wakakusanywa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:6 وَإِذَا ٱلْبِحَارُ سُجِّرَتْ
81:6 Na bahari zikawaka moto, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:7 وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتْ
81:7 Na nafsi zikaunganishwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:8 وَإِذَا ٱلْمَوْءُۥدَةُ سُئِلَتْ
81:8 Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:9 بِأَىِّ ذَنۢبٍ قُتِلَتْ
81:9 Kwa kosa gani aliuliwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:10 وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتْ
81:10 Na madaftari yatakapo enezwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:11 وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتْ
81:11 Na mbingu itapo tanduliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:12 وَإِذَا ٱلْجَحِيمُ سُعِّرَتْ
81:12 Na Jahannamu itapo chochewa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:13 وَإِذَا ٱلْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ
81:13 Na Pepo ikasogezwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:14 عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّآ أَحْضَرَتْ
81:14 Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:15 فَلَآ أُقْسِمُ بِٱلْخُنَّسِ
81:15 Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:16 ٱلْجَوَارِ ٱلْكُنَّسِ
81:16 Zinazo kwenda, kisha zikajificha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:17 وَٱلَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ
81:17 Na kwa usiku unapo pungua, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:18 وَٱلصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ
81:18 Na kwa asubuhi inapo pambazuka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:19 إِنَّهُۥ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ
81:19 Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:20 ذِى قُوَّةٍ عِندَ ذِى ٱلْعَرْشِ مَكِينٍ
81:20 Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:21 مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ
81:21 Anaye t'iiwa, tena muaminifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:22 وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ
81:22 Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:23 وَلَقَدْ رَءَاهُ بِٱلْأُفُقِ ٱلْمُبِينِ
81:23 Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:24 وَمَا هُوَ عَلَى ٱلْغَيْبِ بِضَنِينٍ
81:24 Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:25 وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَـٰنٍ رَّجِيمٍ
81:25 Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:26 فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ
81:26 Basi mnakwenda wapi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:27 إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ
81:27 Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:28 لِمَن شَآءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ
81:28 Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

81:29 وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
81:29 Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)