Selected
Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani
Abdullah Yusuf Ali
Abdul Majid Daryabadi
Abul Ala Maududi
Ahmed Ali
Ahmed Raza Khan
A. J. Arberry
Ali Quli Qarai
Hasan al-Fatih Qaribullah and Ahmad Darwish
Mohammad Habib Shakir
Mohammed Marmaduke William Pickthall
Muhammad Sarwar
Muhammad Taqi-ud-Din al-Hilali and Muhammad Muhsin Khan
Safi-ur-Rahman al-Mubarakpuri
Saheeh International
Talal Itani
Transliteration
Wahiduddin Khan
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.
53:1
وَٱلنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ
53:1
Naapa kwa nyota inapo tua, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:2
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ
53:2
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:3
وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلْهَوَىٰٓ
53:3
Wala hatamki kwa matamanio. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:4
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْىٌ يُوحَىٰ
53:4
Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:5
عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلْقُوَىٰ
53:5
Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:6
ذُو مِرَّةٍ فَٱسْتَوَىٰ
53:6
Mwenye kutua, akatulia, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:7
وَهُوَ بِٱلْأُفُقِ ٱلْأَعْلَىٰ
53:7
Naye yuko juu kabisa upeo wa macho. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:8
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ
53:8
Kisha akakaribia na akateremka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:9
فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ
53:9
Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:10
فَأَوْحَىٰٓ إِلَىٰ عَبْدِهِۦ مَآ أَوْحَىٰ
53:10
Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:11
مَا كَذَبَ ٱلْفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ
53:11
Moyo haukusema uwongo uliyo yaona. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:12
أَفَتُمَـٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ
53:12
Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:13
وَلَقَدْ رَءَاهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ
53:13
Na akamwona mara nyingine, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:14
عِندَ سِدْرَةِ ٱلْمُنتَهَىٰ
53:14
Penye Mkunazi wa mwisho. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:15
عِندَهَا جَنَّةُ ٱلْمَأْوَىٰٓ
53:15
Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:16
إِذْ يَغْشَى ٱلسِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ
53:16
Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:17
مَا زَاغَ ٱلْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ
53:17
Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:18
لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ ءَايَـٰتِ رَبِّهِ ٱلْكُبْرَىٰٓ
53:18
Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:19
أَفَرَءَيْتُمُ ٱللَّـٰتَ وَٱلْعُزَّىٰ
53:19
Je! Mmemuona Lata na Uzza? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:20
وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلْأُخْرَىٰٓ
53:20
Na Manaat, mwingine wa tatu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:21
أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلْأُنثَىٰ
53:21
Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:22
تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰٓ
53:22
Huo ni mgawanyo wa dhulma! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:23
إِنْ هِىَ إِلَّآ أَسْمَآءٌ سَمَّيْتُمُوهَآ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلْطَـٰنٍ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهْوَى ٱلْأَنفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلْهُدَىٰٓ
53:23
Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:24
أَمْ لِلْإِنسَـٰنِ مَا تَمَنَّىٰ
53:24
Ati mtu anakipata kila anacho kitamani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:25
فَلِلَّهِ ٱلْـَٔاخِرَةُ وَٱلْأُولَىٰ
53:25
Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:26
۞ وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ لَا تُغْنِى شَفَـٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعْدِ أَن يَأْذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرْضَىٰٓ
53:26
Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:27
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ تَسْمِيَةَ ٱلْأُنثَىٰ
53:27
Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:28
وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ ۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغْنِى مِنَ ٱلْحَقِّ شَيْـًٔا
53:28
Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:29
فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا
53:29
Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:30
ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ ٱلْعِلْمِ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ ٱهْتَدَىٰ
53:30
Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:31
وَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ لِيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ أَسَـٰٓـُٔوا۟ بِمَا عَمِلُوا۟ وَيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ بِٱلْحُسْنَى
53:31
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:32
ٱلَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَـٰٓئِرَ ٱلْإِثْمِ وَٱلْفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِى بُطُونِ أُمَّهَـٰتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوٓا۟ أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ
53:32
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:33
أَفَرَءَيْتَ ٱلَّذِى تَوَلَّىٰ
53:33
Je! Umemwona yule aliye geuka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:34
وَأَعْطَىٰ قَلِيلًا وَأَكْدَىٰٓ
53:34
Na akatoa kidogo, kisha akajizuia? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:35
أَعِندَهُۥ عِلْمُ ٱلْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ
53:35
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:36
أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِى صُحُفِ مُوسَىٰ
53:36
Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:37
وَإِبْرَٰهِيمَ ٱلَّذِى وَفَّىٰٓ
53:37
Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:38
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ
53:38
Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:39
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَـٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
53:39
Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:40
وَأَنَّ سَعْيَهُۥ سَوْفَ يُرَىٰ
53:40
Na kwamba vitendo vyake vitaonekana? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:41
ثُمَّ يُجْزَىٰهُ ٱلْجَزَآءَ ٱلْأَوْفَىٰ
53:41
Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:42
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلْمُنتَهَىٰ
53:42
Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:43
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ
53:43
Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:44
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا
53:44
Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:45
وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوْجَيْنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰ
53:45
Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:46
مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ
53:46
Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:47
وَأَنَّ عَلَيْهِ ٱلنَّشْأَةَ ٱلْأُخْرَىٰ
53:47
Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:48
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ
53:48
Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:49
وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعْرَىٰ
53:49
Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:50
وَأَنَّهُۥٓ أَهْلَكَ عَادًا ٱلْأُولَىٰ
53:50
Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:51
وَثَمُودَا۟ فَمَآ أَبْقَىٰ
53:51
Na Thamudi hakuwabakisha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:52
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ
53:52
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:53
وَٱلْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ
53:53
Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:54
فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ
53:54
Vikaifunika vilivyo funika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:55
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ
53:55
Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:56
هَـٰذَا نَذِيرٌ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلْأُولَىٰٓ
53:56
Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:57
أَزِفَتِ ٱلْـَٔازِفَةُ
53:57
Kiyama kimekaribia! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:58
لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ
53:58
Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:59
أَفَمِنْ هَـٰذَا ٱلْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ
53:59
Je! Mnayastaajabia maneno haya? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:60
وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ
53:60
Na mnacheka, wala hamlii? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:61
وَأَنتُمْ سَـٰمِدُونَ
53:61
Nanyi mmeghafilika? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
53:62
فَٱسْجُدُوا۟ لِلَّهِ وَٱعْبُدُوا۟ ۩
53:62
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)