Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

91 Ash-Shams ٱلشَّمْس

< Previous   15 Āyah   The Sun      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

91:1 وَٱلشَّمْسِ وَضُحَىٰهَا
91:1 Naapa kwa jua na mwangaza wake! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:2 وَٱلْقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا
91:2 Na kwa mwezi unapo lifuatia! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:3 وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا
91:3 Na kwa mchana unapo lidhihirisha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:4 وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰهَا
91:4 Na kwa usiku unapo lifunika! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:5 وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا
91:5 Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:6 وَٱلْأَرْضِ وَمَا طَحَىٰهَا
91:6 Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:7 وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّىٰهَا
91:7 Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:8 فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَىٰهَا
91:8 Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:9 قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّىٰهَا
91:9 Hakika amefanikiwa aliye itakasa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:10 وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا
91:10 Na hakika amekhasiri aliye iviza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:11 كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَىٰهَآ
91:11 Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:12 إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشْقَىٰهَا
91:12 Alipo simama mwovu wao mkubwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:13 فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقْيَـٰهَا
91:13 Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:14 فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمْ فَسَوَّىٰهَا
91:14 Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

91:15 وَلَا يَخَافُ عُقْبَـٰهَا
91:15 Wala Yeye haogopi matokeo yake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)