Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

38 Şād ص

< Previous   88 Āyah   The Letter "Saad"      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

38:1 صٓ ۚ وَٱلْقُرْءَانِ ذِى ٱلذِّكْرِ
38:1 S'ad, Naapa kwa Qur'ani yenye mawaidha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:2 بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى عِزَّةٍ وَشِقَاقٍ
38:2 Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:3 كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ فَنَادَوا۟ وَّلَاتَ حِينَ مَنَاصٍ
38:3 Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:4 وَعَجِبُوٓا۟ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ ۖ وَقَالَ ٱلْكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا سَـٰحِرٌ كَذَّابٌ
38:4 Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:5 أَجَعَلَ ٱلْـَٔالِهَةَ إِلَـٰهًا وَٰحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَىْءٌ عُجَابٌ
38:5 Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:6 وَٱنطَلَقَ ٱلْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ ٱمْشُوا۟ وَٱصْبِرُوا۟ عَلَىٰٓ ءَالِهَتِكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَىْءٌ يُرَادُ
38:6 Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:7 مَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِى ٱلْمِلَّةِ ٱلْـَٔاخِرَةِ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا ٱخْتِلَـٰقٌ
38:7 Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:8 أَءُنزِلَ عَلَيْهِ ٱلذِّكْرُ مِنۢ بَيْنِنَا ۚ بَلْ هُمْ فِى شَكٍّ مِّن ذِكْرِى ۖ بَل لَّمَّا يَذُوقُوا۟ عَذَابِ
38:8 Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:9 أَمْ عِندَهُمْ خَزَآئِنُ رَحْمَةِ رَبِّكَ ٱلْعَزِيزِ ٱلْوَهَّابِ
38:9 Au wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:10 أَمْ لَهُم مُّلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ فَلْيَرْتَقُوا۟ فِى ٱلْأَسْبَـٰبِ
38:10 Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia za kwendea huko! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:11 جُندٌ مَّا هُنَالِكَ مَهْزُومٌ مِّنَ ٱلْأَحْزَابِ
38:11 Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:12 كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ ذُو ٱلْأَوْتَادِ
38:12 Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:13 وَثَمُودُ وَقَوْمُ لُوطٍ وَأَصْحَـٰبُ لْـَٔيْكَةِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلْأَحْزَابُ
38:13 Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:14 إِن كُلٌّ إِلَّا كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ عِقَابِ
38:14 Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:15 وَمَا يَنظُرُ هَـٰٓؤُلَآءِ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً مَّا لَهَا مِن فَوَاقٍ
38:15 Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:16 وَقَالُوا۟ رَبَّنَا عَجِّل لَّنَا قِطَّنَا قَبْلَ يَوْمِ ٱلْحِسَابِ
38:16 Na wao husema: Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hisabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:17 ٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُۥدَ ذَا ٱلْأَيْدِ ۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ
38:17 Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:18 إِنَّا سَخَّرْنَا ٱلْجِبَالَ مَعَهُۥ يُسَبِّحْنَ بِٱلْعَشِىِّ وَٱلْإِشْرَاقِ
38:18 Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:19 وَٱلطَّيْرَ مَحْشُورَةً ۖ كُلٌّ لَّهُۥٓ أَوَّابٌ
38:19 Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:20 وَشَدَدْنَا مُلْكَهُۥ وَءَاتَيْنَـٰهُ ٱلْحِكْمَةَ وَفَصْلَ ٱلْخِطَابِ
38:20 Na tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa hikima, na kukata hukumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:21 ۞ وَهَلْ أَتَىٰكَ نَبَؤُا۟ ٱلْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا۟ ٱلْمِحْرَابَ
38:21 Na je! Imekufikia khabari ya wagombanao walipo pindukia ukuta kuingia chumbani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:22 إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَىٰ دَاوُۥدَ فَفَزِعَ مِنْهُمْ ۖ قَالُوا۟ لَا تَخَفْ ۖ خَصْمَانِ بَغَىٰ بَعْضُنَا عَلَىٰ بَعْضٍ فَٱحْكُم بَيْنَنَا بِٱلْحَقِّ وَلَا تُشْطِطْ وَٱهْدِنَآ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلصِّرَٰطِ
38:22 Walipo muingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:23 إِنَّ هَـٰذَآ أَخِى لَهُۥ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ نَعْجَةً وَلِىَ نَعْجَةٌ وَٰحِدَةٌ فَقَالَ أَكْفِلْنِيهَا وَعَزَّنِى فِى ٱلْخِطَابِ
38:23 Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisiini na tisa; na mimi ninaye kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo nikufugie! Na amenishinda kwa maneno. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:24 قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦ ۖ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْخُلَطَآءِ لَيَبْغِى بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ ۗ وَظَنَّ دَاوُۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّـٰهُ فَٱسْتَغْفَرَ رَبَّهُۥ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ۩
38:24 Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:25 فَغَفَرْنَا لَهُۥ ذَٰلِكَ ۖ وَإِنَّ لَهُۥ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَـَٔابٍ
38:25 Basi tukamsamehe kwa hayo. Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo mazuri kwetu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:26 يَـٰدَاوُۥدُ إِنَّا جَعَلْنَـٰكَ خَلِيفَةً فِى ٱلْأَرْضِ فَٱحْكُم بَيْنَ ٱلنَّاسِ بِٱلْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعِ ٱلْهَوَىٰ فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَضِلُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌۢ بِمَا نَسُوا۟ يَوْمَ ٱلْحِسَابِ
38:26 Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:27 وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَآءَ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَـٰطِلًا ۚ ذَٰلِكَ ظَنُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۚ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنَ ٱلنَّارِ
38:27 Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yao bure. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:28 أَمْ نَجْعَلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ كَٱلْمُفْسِدِينَ فِى ٱلْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ ٱلْمُتَّقِينَ كَٱلْفُجَّارِ
38:28 Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wachamngu kama waovu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:29 كِتَـٰبٌ أَنزَلْنَـٰهُ إِلَيْكَ مُبَـٰرَكٌ لِّيَدَّبَّرُوٓا۟ ءَايَـٰتِهِۦ وَلِيَتَذَكَّرَ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ
38:29 Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:30 وَوَهَبْنَا لِدَاوُۥدَ سُلَيْمَـٰنَ ۚ نِعْمَ ٱلْعَبْدُ ۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ
38:30 Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:31 إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِٱلْعَشِىِّ ٱلصَّـٰفِنَـٰتُ ٱلْجِيَادُ
38:31 Alipo pelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:32 فَقَالَ إِنِّىٓ أَحْبَبْتُ حُبَّ ٱلْخَيْرِ عَن ذِكْرِ رَبِّى حَتَّىٰ تَوَارَتْ بِٱلْحِجَابِ
38:32 Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha wakafichikana nyuma ya boma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:33 رُدُّوهَا عَلَىَّ ۖ فَطَفِقَ مَسْحًۢا بِٱلسُّوقِ وَٱلْأَعْنَاقِ
38:33 (Akasema:) Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:34 وَلَقَدْ فَتَنَّا سُلَيْمَـٰنَ وَأَلْقَيْنَا عَلَىٰ كُرْسِيِّهِۦ جَسَدًا ثُمَّ أَنَابَ
38:34 Na tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:35 قَالَ رَبِّ ٱغْفِرْ لِى وَهَبْ لِى مُلْكًا لَّا يَنۢبَغِى لِأَحَدٍ مِّنۢ بَعْدِىٓ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ
38:35 Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:36 فَسَخَّرْنَا لَهُ ٱلرِّيحَ تَجْرِى بِأَمْرِهِۦ رُخَآءً حَيْثُ أَصَابَ
38:36 Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:37 وَٱلشَّيَـٰطِينَ كُلَّ بَنَّآءٍ وَغَوَّاصٍ
38:37 Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:38 وَءَاخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِى ٱلْأَصْفَادِ
38:38 Na wengine wafungwao kwa minyororo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:39 هَـٰذَا عَطَآؤُنَا فَٱمْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ
38:39 Hichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:40 وَإِنَّ لَهُۥ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَـَٔابٍ
38:40 Na hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:41 وَٱذْكُرْ عَبْدَنَآ أَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلشَّيْطَـٰنُ بِنُصْبٍ وَعَذَابٍ
38:41 Na mkumbuke mja wetu Ayubu alipo mwita Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika Shet'ani amenifikishia udhia na adhabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:42 ٱرْكُضْ بِرِجْلِكَ ۖ هَـٰذَا مُغْتَسَلٌۢ بَارِدٌ وَشَرَابٌ
38:42 (Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:43 وَوَهَبْنَا لَهُۥٓ أَهْلَهُۥ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنَّا وَذِكْرَىٰ لِأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ
38:43 Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:44 وَخُذْ بِيَدِكَ ضِغْثًا فَٱضْرِب بِّهِۦ وَلَا تَحْنَثْ ۗ إِنَّا وَجَدْنَـٰهُ صَابِرًا ۚ نِّعْمَ ٱلْعَبْدُ ۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ
38:44 Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:45 وَٱذْكُرْ عِبَـٰدَنَآ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ أُو۟لِى ٱلْأَيْدِى وَٱلْأَبْصَـٰرِ
38:45 Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu walio kuwa na nguvu na busara. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:46 إِنَّآ أَخْلَصْنَـٰهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى ٱلدَّارِ
38:46 Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:47 وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ ٱلْمُصْطَفَيْنَ ٱلْأَخْيَارِ
38:47 Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:48 وَٱذْكُرْ إِسْمَـٰعِيلَ وَٱلْيَسَعَ وَذَا ٱلْكِفْلِ ۖ وَكُلٌّ مِّنَ ٱلْأَخْيَارِ
38:48 Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:49 هَـٰذَا ذِكْرٌ ۚ وَإِنَّ لِلْمُتَّقِينَ لَحُسْنَ مَـَٔابٍ
38:49 Huu ni ukumbusho. Na hakika wachamngu wana marudio mazuri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:50 جَنَّـٰتِ عَدْنٍ مُّفَتَّحَةً لَّهُمُ ٱلْأَبْوَٰبُ
38:50 Bustani za milele zitazo funguliwa milango yao kwa ajili yao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:51 مُتَّكِـِٔينَ فِيهَا يَدْعُونَ فِيهَا بِفَـٰكِهَةٍ كَثِيرَةٍ وَشَرَابٍ
38:51 Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:52 ۞ وَعِندَهُمْ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ أَتْرَابٌ
38:52 Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:53 هَـٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِيَوْمِ ٱلْحِسَابِ
38:53 Haya ndiyo mliyo ahidiwa kwa Siku ya Hisabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:54 إِنَّ هَـٰذَا لَرِزْقُنَا مَا لَهُۥ مِن نَّفَادٍ
38:54 Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyo malizika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:55 هَـٰذَا ۚ وَإِنَّ لِلطَّـٰغِينَ لَشَرَّ مَـَٔابٍ
38:55 Ndio hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:56 جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ
38:56 Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:57 هَـٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ
38:57 Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:58 وَءَاخَرُ مِن شَكْلِهِۦٓ أَزْوَٰجٌ
38:58 Na adhabu nyenginezo za namna hii. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:59 هَـٰذَا فَوْجٌ مُّقْتَحِمٌ مَّعَكُمْ ۖ لَا مَرْحَبًۢا بِهِمْ ۚ إِنَّهُمْ صَالُوا۟ ٱلنَّارِ
38:59 Hili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:60 قَالُوا۟ بَلْ أَنتُمْ لَا مَرْحَبًۢا بِكُمْ ۖ أَنتُمْ قَدَّمْتُمُوهُ لَنَا ۖ فَبِئْسَ ٱلْقَرَارُ
38:60 Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mlio tusabibisha haya, napo ni pahala paovu kabisa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:61 قَالُوا۟ رَبَّنَا مَن قَدَّمَ لَنَا هَـٰذَا فَزِدْهُ عَذَابًا ضِعْفًا فِى ٱلنَّارِ
38:61 Waseme: Mola wetu Mlezi! Aliye tusabibisha haya mzidishie adhabu mara mbili Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:62 وَقَالُوا۟ مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ ٱلْأَشْرَارِ
38:62 Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:63 أَتَّخَذْنَـٰهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ ٱلْأَبْصَـٰرُ
38:63 Tulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:64 إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقٌّ تَخَاصُمُ أَهْلِ ٱلنَّارِ
38:64 Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:65 قُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ مُنذِرٌ ۖ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّارُ
38:65 Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:66 رَبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ٱلْعَزِيزُ ٱلْغَفَّـٰرُ
38:66 Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:67 قُلْ هُوَ نَبَؤٌا۟ عَظِيمٌ
38:67 Sema: Hii ni khabari kubwa kabisa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:68 أَنتُمْ عَنْهُ مُعْرِضُونَ
38:68 Ambayo nyinyi mnaipuuza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:69 مَا كَانَ لِىَ مِنْ عِلْمٍۭ بِٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰٓ إِذْ يَخْتَصِمُونَ
38:69 Sikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipo kuwa wakishindana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:70 إِن يُوحَىٰٓ إِلَىَّ إِلَّآ أَنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
38:70 Haikufunuliwa kwangu isipo kuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhaahiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:71 إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى خَـٰلِقٌۢ بَشَرًا مِّن طِينٍ
38:71 Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:72 فَإِذَا سَوَّيْتُهُۥ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُوا۟ لَهُۥ سَـٰجِدِينَ
38:72 Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:73 فَسَجَدَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ
38:73 Basi Malaika wakat'ii wote pamoja. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:74 إِلَّآ إِبْلِيسَ ٱسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ
38:74 Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:75 قَالَ يَـٰٓإِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَىَّ ۖ أَسْتَكْبَرْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ ٱلْعَالِينَ
38:75 Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:76 قَالَ أَنَا۠ خَيْرٌ مِّنْهُ ۖ خَلَقْتَنِى مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُۥ مِن طِينٍ
38:76 Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:77 قَالَ فَٱخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ
38:77 Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:78 وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِىٓ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلدِّينِ
38:78 Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:79 قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِىٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
38:79 Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:80 قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلْمُنظَرِينَ
38:80 Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:81 إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْوَقْتِ ٱلْمَعْلُومِ
38:81 Mpaka siku ya wakati maalumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:82 قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
38:82 Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:83 إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ ٱلْمُخْلَصِينَ
38:83 Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:84 قَالَ فَٱلْحَقُّ وَٱلْحَقَّ أَقُولُ
38:84 Akasema: Haki! Na haki ninaisema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:85 لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكَ وَمِمَّن تَبِعَكَ مِنْهُمْ أَجْمَعِينَ
38:85 Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:86 قُلْ مَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُتَكَلِّفِينَ
38:86 Sema (Ewe Mtume): Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:87 إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ
38:87 Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

38:88 وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُۥ بَعْدَ حِينٍۭ
38:88 Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)