Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

36 Yā-Sīn يس

< Previous   83 Āyah   Ya Sin      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

36:1 يسٓ
36:1 Ya-Sin (Y. S.). - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:2 وَٱلْقُرْءَانِ ٱلْحَكِيمِ
36:2 Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:3 إِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
36:3 Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:4 عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
36:4 Juu ya Njia Iliyo Nyooka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:5 تَنزِيلَ ٱلْعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ
36:5 Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:6 لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمْ فَهُمْ غَـٰفِلُونَ
36:6 Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:7 لَقَدْ حَقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَىٰٓ أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
36:7 Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:8 إِنَّا جَعَلْنَا فِىٓ أَعْنَـٰقِهِمْ أَغْلَـٰلًا فَهِىَ إِلَى ٱلْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ
36:8 Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:9 وَجَعَلْنَا مِنۢ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَـٰهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ
36:9 Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:10 وَسَوَآءٌ عَلَيْهِمْ ءَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
36:10 Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:11 إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّكْرَ وَخَشِىَ ٱلرَّحْمَـٰنَ بِٱلْغَيْبِ ۖ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَةٍ وَأَجْرٍ كَرِيمٍ
36:11 Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:12 إِنَّا نَحْنُ نُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا۟ وَءَاثَـٰرَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَـٰهُ فِىٓ إِمَامٍ مُّبِينٍ
36:12 Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:13 وَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا أَصْحَـٰبَ ٱلْقَرْيَةِ إِذْ جَآءَهَا ٱلْمُرْسَلُونَ
36:13 Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:14 إِذْ أَرْسَلْنَآ إِلَيْهِمُ ٱثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِثٍ فَقَالُوٓا۟ إِنَّآ إِلَيْكُم مُّرْسَلُونَ
36:14 Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:15 قَالُوا۟ مَآ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَمَآ أَنزَلَ ٱلرَّحْمَـٰنُ مِن شَىْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَكْذِبُونَ
36:15 Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:16 قَالُوا۟ رَبُّنَا يَعْلَمُ إِنَّآ إِلَيْكُمْ لَمُرْسَلُونَ
36:16 Wakasema: Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:17 وَمَا عَلَيْنَآ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ
36:17 Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:18 قَالُوٓا۟ إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهُوا۟ لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ
36:18 Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:19 قَالُوا۟ طَـٰٓئِرُكُم مَّعَكُمْ ۚ أَئِن ذُكِّرْتُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ
36:19 Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukia mipaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:20 وَجَآءَ مِنْ أَقْصَا ٱلْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَىٰ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱتَّبِعُوا۟ ٱلْمُرْسَلِينَ
36:20 Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni hawa walio tumwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:21 ٱتَّبِعُوا۟ مَن لَّا يَسْـَٔلُكُمْ أَجْرًا وَهُم مُّهْتَدُونَ
36:21 Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:22 وَمَا لِىَ لَآ أَعْبُدُ ٱلَّذِى فَطَرَنِى وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
36:22 NA KWA NINI nisimuabudu yule aliye niumba na kwake mtarejeshwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:23 ءَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً إِن يُرِدْنِ ٱلرَّحْمَـٰنُ بِضُرٍّ لَّا تُغْنِ عَنِّى شَفَـٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا يُنقِذُونِ
36:23 Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:24 إِنِّىٓ إِذًا لَّفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ
36:24 Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:25 إِنِّىٓ ءَامَنتُ بِرَبِّكُمْ فَٱسْمَعُونِ
36:25 Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:26 قِيلَ ٱدْخُلِ ٱلْجَنَّةَ ۖ قَالَ يَـٰلَيْتَ قَوْمِى يَعْلَمُونَ
36:26 Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:27 بِمَا غَفَرَ لِى رَبِّى وَجَعَلَنِى مِنَ ٱلْمُكْرَمِينَ
36:27 Jinsi Mola wangu Mlezi alivyo nisamehe, na akanifanya miongoni mwa walio hishimiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:28 ۞ وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَىٰ قَوْمِهِۦ مِنۢ بَعْدِهِۦ مِن جُندٍ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ
36:28 Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:29 إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ خَـٰمِدُونَ
36:29 Hakukuwa ila ukelele mmoja tu; na mara walizimwa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:30 يَـٰحَسْرَةً عَلَى ٱلْعِبَادِ ۚ مَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
36:30 Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:31 أَلَمْ يَرَوْا۟ كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ ٱلْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لَا يَرْجِعُونَ
36:31 Je! Hawaoni umma ngapi tulizo ziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:32 وَإِن كُلٌّ لَّمَّا جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ
36:32 Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:33 وَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلْأَرْضُ ٱلْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَـٰهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ
36:33 Na Ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazila! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:34 وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّـٰتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَـٰبٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ ٱلْعُيُونِ
36:34 Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:35 لِيَأْكُلُوا۟ مِن ثَمَرِهِۦ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ
36:35 Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:36 سُبْحَـٰنَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلْأَزْوَٰجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلْأَرْضُ وَمِنْ أَنفُسِهِمْ وَمِمَّا لَا يَعْلَمُونَ
36:36 Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:37 وَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ ٱلنَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظْلِمُونَ
36:37 Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:38 وَٱلشَّمْسُ تَجْرِى لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ
36:38 Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:39 وَٱلْقَمَرَ قَدَّرْنَـٰهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَٱلْعُرْجُونِ ٱلْقَدِيمِ
36:39 Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:40 لَا ٱلشَّمْسُ يَنۢبَغِى لَهَآ أَن تُدْرِكَ ٱلْقَمَرَ وَلَا ٱلَّيْلُ سَابِقُ ٱلنَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِى فَلَكٍ يَسْبَحُونَ
36:40 Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:41 وَءَايَةٌ لَّهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ
36:41 Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:42 وَخَلَقْنَا لَهُم مِّن مِّثْلِهِۦ مَا يَرْكَبُونَ
36:42 Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyo vipanda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:43 وَإِن نَّشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلَا صَرِيخَ لَهُمْ وَلَا هُمْ يُنقَذُونَ
36:43 Na tukitaka tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:44 إِلَّا رَحْمَةً مِّنَّا وَمَتَـٰعًا إِلَىٰ حِينٍ
36:44 Isipo kuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:45 وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّقُوا۟ مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
36:45 Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa... - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:46 وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ ءَايَةٍ مِّنْ ءَايَـٰتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهَا مُعْرِضِينَ
36:46 Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:47 وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنفِقُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنُطْعِمُ مَن لَّوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ أَطْعَمَهُۥٓ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ
36:47 Na wanapo ambiwa: Toeni katika aliyo kupeni Mwenyezi Mungu, walio kufuru huwaambia walio amini: Je! Tuwalishe ambao Mwenyezi Mungu angependa angeli walisha mwenyewe? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhaahiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:48 وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
36:48 Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:49 مَا يَنظُرُونَ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ
36:49 Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukua nao wamo kuzozana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:50 فَلَا يَسْتَطِيعُونَ تَوْصِيَةً وَلَآ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمْ يَرْجِعُونَ
36:50 Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:51 وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ ٱلْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ
36:51 Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:52 قَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا مَنۢ بَعَثَنَا مِن مَّرْقَدِنَا ۜ ۗ هَـٰذَا مَا وَعَدَ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَصَدَقَ ٱلْمُرْسَلُونَ
36:52 Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:53 إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ
36:53 Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhuruishwa mbele yetu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:54 فَٱلْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْـًٔا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
36:54 Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:55 إِنَّ أَصْحَـٰبَ ٱلْجَنَّةِ ٱلْيَوْمَ فِى شُغُلٍ فَـٰكِهُونَ
36:55 Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:56 هُمْ وَأَزْوَٰجُهُمْ فِى ظِلَـٰلٍ عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ مُتَّكِـُٔونَ
36:56 Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fakhari. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:57 لَهُمْ فِيهَا فَـٰكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ
36:57 Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakacho kitaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:58 سَلَـٰمٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ
36:58 "Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:59 وَٱمْتَـٰزُوا۟ ٱلْيَوْمَ أَيُّهَا ٱلْمُجْرِمُونَ
36:59 Na enyi wakosefu! Jitengeni leo! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:60 ۞ أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا۟ ٱلشَّيْطَـٰنَ ۖ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ
36:60 Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwa msimuabudu Shet'ani? Hakika yeye ni adui dhaahiri kwenu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:61 وَأَنِ ٱعْبُدُونِى ۚ هَـٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ
36:61 Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:62 وَلَقَدْ أَضَلَّ مِنكُمْ جِبِلًّا كَثِيرًا ۖ أَفَلَمْ تَكُونُوا۟ تَعْقِلُونَ
36:62 Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:63 هَـٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِى كُنتُمْ تُوعَدُونَ
36:63 Hii basi ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:64 ٱصْلَوْهَا ٱلْيَوْمَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ
36:64 Ingieni leo kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:65 ٱلْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰٓ أَفْوَٰهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَآ أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
36:65 Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyachuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:66 وَلَوْ نَشَآءُ لَطَمَسْنَا عَلَىٰٓ أَعْيُنِهِمْ فَٱسْتَبَقُوا۟ ٱلصِّرَٰطَ فَأَنَّىٰ يُبْصِرُونَ
36:66 Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:67 وَلَوْ نَشَآءُ لَمَسَخْنَـٰهُمْ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمْ فَمَا ٱسْتَطَـٰعُوا۟ مُضِيًّا وَلَا يَرْجِعُونَ
36:67 Na tungeli taka tunge wageuza sura hapo hapo walipo, basi wasinge weza kwenda wala kurudi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:68 وَمَن نُّعَمِّرْهُ نُنَكِّسْهُ فِى ٱلْخَلْقِ ۖ أَفَلَا يَعْقِلُونَ
36:68 Na tunaye mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:69 وَمَا عَلَّمْنَـٰهُ ٱلشِّعْرَ وَمَا يَنۢبَغِى لَهُۥٓ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْءَانٌ مُّبِينٌ
36:69 Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:70 لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيًّا وَيَحِقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ
36:70 Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:71 أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَآ أَنْعَـٰمًا فَهُمْ لَهَا مَـٰلِكُونَ
36:71 Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyo fanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:72 وَذَلَّلْنَـٰهَا لَهُمْ فَمِنْهَا رَكُوبُهُمْ وَمِنْهَا يَأْكُلُونَ
36:72 Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanao wapanda, na baadhi yao wanawala. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:73 وَلَهُمْ فِيهَا مَنَـٰفِعُ وَمَشَارِبُ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ
36:73 Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:74 وَٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ ءَالِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ
36:74 Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:75 لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ
36:75 Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakao hudhurishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:76 فَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّا نَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ
36:76 Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaweka siri na wanayo yatangaza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:77 أَوَلَمْ يَرَ ٱلْإِنسَـٰنُ أَنَّا خَلَقْنَـٰهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ
36:77 Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:78 وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِىَ خَلْقَهُۥ ۖ قَالَ مَن يُحْىِ ٱلْعِظَـٰمَ وَهِىَ رَمِيمٌ
36:78 Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:79 قُلْ يُحْيِيهَا ٱلَّذِىٓ أَنشَأَهَآ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ
36:79 Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:80 ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلشَّجَرِ ٱلْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَآ أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ
36:80 Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:81 أَوَلَيْسَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِقَـٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ۚ بَلَىٰ وَهُوَ ٱلْخَلَّـٰقُ ٱلْعَلِيمُ
36:81 Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:82 إِنَّمَآ أَمْرُهُۥٓ إِذَآ أَرَادَ شَيْـًٔا أَن يَقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
36:82 Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

36:83 فَسُبْحَـٰنَ ٱلَّذِى بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَىْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
36:83 Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)