Selected
                        Original Text
                        
                    
                
                    
                        Ali Muhsin Al-Barwani
                        
                        
                        
                    
                
                Abdullah Yusuf Ali
Abdul Majid Daryabadi
Abul Ala Maududi
Ahmed Ali
Ahmed Raza Khan
A. J. Arberry
Ali Quli Qarai
Hasan al-Fatih Qaribullah and Ahmad Darwish
Mohammad Habib Shakir
Mohammed Marmaduke William Pickthall
Muhammad Sarwar
Muhammad Taqi-ud-Din al-Hilali and Muhammad Muhsin Khan
Safi-ur-Rahman al-Mubarakpuri
Saheeh International
Talal Itani
Transliteration
Wahiduddin Khan
                    بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
                
                
                    In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.
                
            
                    52:1
                    وَٱلطُّورِ
                
                
                
                
                
                    52:1
                    Naapa kwa mlima wa T'ur,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:2
                    وَكِتَـٰبٍ مَّسْطُورٍ
                
                
                
                
                
                    52:2
                    Na Kitabu kilicho andikwa  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:3
                    فِى رَقٍّ مَّنشُورٍ
                
                
                
                
                
                    52:3
                    Katika ngozi iliyo kunjuliwa,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:4
                    وَٱلْبَيْتِ ٱلْمَعْمُورِ
                
                
                
                
                
                    52:4
                    Na kwa Nyumba iliyo jengwa,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:5
                    وَٱلسَّقْفِ ٱلْمَرْفُوعِ
                
                
                
                
                
                    52:5
                    Na kwa dari iliyo nyanyuliwa,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:6
                    وَٱلْبَحْرِ ٱلْمَسْجُورِ
                
                
                
                
                
                    52:6
                    Na kwa bahari iliyo jazwa,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:7
                    إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعٌ
                
                
                
                
                
                    52:7
                    Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:8
                    مَّا لَهُۥ مِن دَافِعٍ
                
                
                
                
                
                    52:8
                    Hapana wa kuizuia.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:9
                    يَوْمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوْرًا
                
                
                
                
                
                    52:9
                    Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:10
                    وَتَسِيرُ ٱلْجِبَالُ سَيْرًا
                
                
                
                
                
                    52:10
                    Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:11
                    فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
                
                
                
                
                
                    52:11
                    Basi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:12
                    ٱلَّذِينَ هُمْ فِى خَوْضٍ يَلْعَبُونَ
                
                
                
                
                
                    52:12
                    Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:13
                    يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا
                
                
                
                
                
                    52:13
                    Siku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:14
                    هَـٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِى كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ
                
                
                
                
                
                    52:14
                    (Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha!  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:15
                    أَفَسِحْرٌ هَـٰذَآ أَمْ أَنتُمْ لَا تُبْصِرُونَ
                
                
                
                
                
                    52:15
                    Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu?  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:16
                    ٱصْلَوْهَا فَٱصْبِرُوٓا۟ أَوْ لَا تَصْبِرُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْكُمْ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
                
                
                
                
                
                    52:16
                    Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:17
                    إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَنَعِيمٍ
                
                
                
                
                
                    52:17
                    Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:18
                    فَـٰكِهِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَىٰهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ
                
                
                
                
                
                    52:18
                    Wakifurahi kwa yale aliyo wapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:19
                    كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
                
                
                
                
                
                    52:19
                    Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyatenda.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:20
                    مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ ۖ وَزَوَّجْنَـٰهُم بِحُورٍ عِينٍ
                
                
                
                
                
                    52:20
                    Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:21
                    وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَـٰنٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَآ أَلَتْنَـٰهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَىْءٍ ۚ كُلُّ ٱمْرِئٍۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ
                
                
                
                
                
                    52:21
                    Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:22
                    وَأَمْدَدْنَـٰهُم بِفَـٰكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ
                
                
                
                
                
                    52:22
                    Na tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:23
                    يَتَنَـٰزَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ
                
                
                
                
                
                    52:23
                    Watapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:24
                    ۞ وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَّهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَّكْنُونٌ
                
                
                
                
                
                    52:24
                    Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:25
                    وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ
                
                
                
                
                
                    52:25
                    Wataelekeana wakiulizana.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:26
                    قَالُوٓا۟ إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِىٓ أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ
                
                
                
                
                
                    52:26
                    Waseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa;  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:27
                    فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْنَا وَوَقَىٰنَا عَذَابَ ٱلسَّمُومِ
                
                
                
                
                
                    52:27
                    Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:28
                    إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْبَرُّ ٱلرَّحِيمُ
                
                
                
                
                
                    52:28
                    Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:29
                    فَذَكِّرْ فَمَآ أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ
                
                
                
                
                
                    52:29
                    Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:30
                    أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَّتَرَبَّصُ بِهِۦ رَيْبَ ٱلْمَنُونِ
                
                
                
                
                
                    52:30
                    Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:31
                    قُلْ تَرَبَّصُوا۟ فَإِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُتَرَبِّصِينَ
                
                
                
                
                
                    52:31
                    Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:32
                    أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَـٰمُهُم بِهَـٰذَآ ۚ أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ
                
                
                
                
                
                    52:32
                    Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:33
                    أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُۥ ۚ بَل لَّا يُؤْمِنُونَ
                
                
                
                
                
                    52:33
                    Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini!  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:34
                    فَلْيَأْتُوا۟ بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِۦٓ إِن كَانُوا۟ صَـٰدِقِينَ
                
                
                
                
                
                    52:34
                    Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:35
                    أَمْ خُلِقُوا۟ مِنْ غَيْرِ شَىْءٍ أَمْ هُمُ ٱلْخَـٰلِقُونَ
                
                
                
                
                
                    52:35
                    Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:36
                    أَمْ خَلَقُوا۟ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ
                
                
                
                
                
                    52:36
                    Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:37
                    أَمْ عِندَهُمْ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ ٱلْمُصَۣيْطِرُونَ
                
                
                
                
                
                    52:37
                    Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:38
                    أَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ ۖ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُم بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ
                
                
                
                
                
                    52:38
                    Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi!  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:39
                    أَمْ لَهُ ٱلْبَنَـٰتُ وَلَكُمُ ٱلْبَنُونَ
                
                
                
                
                
                    52:39
                    Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana?  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:40
                    أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ
                
                
                
                
                
                    52:40
                    Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:41
                    أَمْ عِندَهُمُ ٱلْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
                
                
                
                
                
                    52:41
                    Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika?  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:42
                    أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدًا ۖ فَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هُمُ ٱلْمَكِيدُونَ
                
                
                
                
                
                    52:42
                    Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:43
                    أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ ۚ سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ
                
                
                
                
                
                    52:43
                    Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:44
                    وَإِن يَرَوْا۟ كِسْفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ سَاقِطًا يَقُولُوا۟ سَحَابٌ مَّرْكُومٌ
                
                
                
                
                
                    52:44
                    Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:45
                    فَذَرْهُمْ حَتَّىٰ يُلَـٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى فِيهِ يُصْعَقُونَ
                
                
                
                
                
                    52:45
                    Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:46
                    يَوْمَ لَا يُغْنِى عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ
                
                
                
                
                
                    52:46
                    Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:47
                    وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ عَذَابًا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
                
                
                
                
                
                    52:47
                    Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:48
                    وَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ
                
                
                
                
                
                    52:48
                    Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama,  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
                
                
                
                
                
                    52:49
                    وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَـٰرَ ٱلنُّجُومِ
                
                
                
                
                
                    52:49
                    Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota.  - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)