Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

73 Al-Muzzammil ٱلْمُزَّمِّل

< Previous   20 Āyah   The Enshrouded One      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

73:1 يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمُزَّمِّلُ
73:1 Ewe uliye jifunika! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:2 قُمِ ٱلَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا
73:2 Kesha usiku kucha, ila kidogo tu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:3 نِّصْفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا
73:3 Nusu yake, au ipunguze kidogo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:4 أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ ٱلْقُرْءَانَ تَرْتِيلًا
73:4 Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:5 إِنَّا سَنُلْقِى عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا
73:5 Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:6 إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيْلِ هِىَ أَشَدُّ وَطْـًٔا وَأَقْوَمُ قِيلًا
73:6 Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:7 إِنَّ لَكَ فِى ٱلنَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا
73:7 Kwani hakika mchana una shughuli nyingi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:8 وَٱذْكُرِ ٱسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا
73:8 Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:9 رَّبُّ ٱلْمَشْرِقِ وَٱلْمَغْرِبِ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذْهُ وَكِيلًا
73:9 Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipo kuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:10 وَٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا
73:10 Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:11 وَذَرْنِى وَٱلْمُكَذِّبِينَ أُو۟لِى ٱلنَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا
73:11 Na niache Mimi na hao wanao kanusha, walio neemeka; na wape muhula kidogo! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:12 إِنَّ لَدَيْنَآ أَنكَالًا وَجَحِيمًا
73:12 Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:13 وَطَعَامًا ذَا غُصَّةٍ وَعَذَابًا أَلِيمًا
73:13 Na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:14 يَوْمَ تَرْجُفُ ٱلْأَرْضُ وَٱلْجِبَالُ وَكَانَتِ ٱلْجِبَالُ كَثِيبًا مَّهِيلًا
73:14 Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:15 إِنَّآ أَرْسَلْنَآ إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَـٰهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَآ أَرْسَلْنَآ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا
73:15 Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:16 فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ ٱلرَّسُولَ فَأَخَذْنَـٰهُ أَخْذًا وَبِيلًا
73:16 Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:17 فَكَيْفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرْتُمْ يَوْمًا يَجْعَلُ ٱلْوِلْدَٰنَ شِيبًا
73:17 Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:18 ٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرٌۢ بِهِۦ ۚ كَانَ وَعْدُهُۥ مَفْعُولًا
73:18 Hapo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:19 إِنَّ هَـٰذِهِۦ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا
73:19 Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

73:20 ۞ إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَىِ ٱلَّيْلِ وَنِصْفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٌ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ فَٱقْرَءُوا۟ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلْقُرْءَانِ ۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ ۙ وَءَاخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِى ٱلْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ ٱللَّهِ ۙ وَءَاخَرُونَ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ فَٱقْرَءُوا۟ مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ ۚ وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقْرِضُوا۟ ٱللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا۟ لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ وَٱسْتَغْفِرُوا۟ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌۢ
73:20 Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)